Ruzuku ya bilioni 100 yashusha bei ya mafuta

0
2290


Ruzuku ya bilioni 100 yashusha bei ya mafuta Ruzuku ya shilingi bilioni 100 iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhibuti ukali wa upandaji wa bei ya mafuta, na kupunguza madhara kwa wananchi.

Taarifa ya EWURA imeonesha kuwa katika fedha hizo kwenye kila lita moja ya petroli na dizeli serikali imetoa ruzuku ya shilingi 306 na 320 mtawalia kwa mafuta yaliyopita Bandari ya Dar es Salaam.

Kutokana na ruzuku hiyo, kwa mkoa wa Dar es Salaam bei ya petroli na dizeli zimeshuka kufikia shilingi 2,994 na shilingi 3,131 mtawalia huku mafuta ya taa yakiwa shilingi 3,299.

Bei za mafuta katika soko la dunia zimeongezeka zaidi kutokana, pamoja na mambo mengine, vita kati ya Urusi na Ukraine ambayo imeathiri mfumo wa usambazaji wa mafuta kutokan na vikwazo.

Pakua hapa chini taarifa ya EWURA kuona bei kwa mikoa yote.