NGOZI: Zao lenye thamani kubwa

0
282

Mwenyekiti Chama cha Uendeshaji Mifugo Tanzania aeleza umuhimu wa lishe katika zao la ngozi leo alipokuwa kwenye mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania.

Dkt. Daniel Komwihangilo amesema bidhaa bora za ngozi zinatokana na ngozi itokanayo na mnyama aliyepata lishe bora.

“Wataalam ambao wanahusiana na mambo ya lishe wanahakikisha kwamba mnyama analishwa vizuri ili hatimaye ngozi iwe vizuri,” ameongeza Dkt. Komwihangilo.

Aidha, amesema kuwa uwekaji wa alama katika ngozi za wanyama unapaswa kuwekwa kwa umakini ili kuepuka kushusha thamani ya ngozi.

Mbali na matumizi ya ngozi kutumika kutengeneza bidhaa kama mikanda, viatu na pochi, yapo baadhi ya makabila duniani ikiwemo nchini Nigeria ambapo ngozi ya ng’ombe hutumika kama chakula (Ponmo).