Mteja anapunguziwa bei asipodai risiti

0
515

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amezitaja changamoto katika masuala ya kujenga uchumi na kukuza ukusanyaji wa mapato ya ndani.

Akizungumza katika Jukwaa la Kodi na Uwekezaji la Mwaka 2024 jijini Dar es Salaam, amesema ulipaji wa kodi kwa hiari ni mdogo na unakumbuna na visingizio vingi kwani suala la kutoa risiti linatumika kama punguzo kwa muuzaji wa bidhaa anapotaka kumuuzia mnunuzi kwa bei nafuu.

Amesema mnunuzi anapouziwa bidhaa hupewa bei tofauti kulingana na kama atahitaji risiti au la. Ikiwa atahitaji risiti, hatopata punguzo la bei, hivyo kupelekea mnunuzi kuongozwa kukwepa kodi kwa kupewa bei isiyo ya risiti ambayo ni punguzo la bidhaa anayonunua.

Changamoto nyingine amesema vipo visingizio vingi kuhusu mifumo ya TEHAMA, ambapo wauzaji husema mfumo upo chini au mashine zimeharibika na kwamba hiyo ni njia mojawapo inayotumika kuuza bidhaa bila ya kutoa risiti za kodi.

Amesema suala hilo sehemu nyingi linatumika kwa makusudi.