Mazingira ya uwekezaji Zanzibar yawavutia Wawekezaji

0
226

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi amesema serikali inahitaji uwepo wa shughuli za uwekezaji ili kuharakisha kasi ya maendeleo na kukuza uchumi.

Dkt Mwinyi amesema hayo Ikulu jijini Zanzibar, alipokutana na ujumbe wa Wawekezaji kutoka kampuni ya Ozuaydin  ya Uturuki ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Mahmet Aydin,  ambao wameonesha nia ya kuwekeza katika ujenzi wa bandari, uwekaji wa vifaa pamoja na uendeshaji wa shughuli za bandari  katika eneo la Malindi na Mpigaduri.

Amesema serikali iko tayari kushirikiana na wawekezaji kuhakikisha inaweka mazingira mazuri yanayovutia ili kufanikisha azma hiyo na kuwataka wawekezaji hao kuwasiliana na mamlaka zinazosimamia uwekezaji ili kupata miongozo na taratibu za kisheria zinazohusu jambo hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo ya Uzuaydin,-Mahmet Aydin amesema wamedhamiria kutumia fursa za uwekezaji  zilizopo nchini baada ya kuridhishwa na mazingira bora yaliopo.

Amesema uwekezaji wanaolenga kuufanya utakuwa na tija na maslahi kwa wananchi wa Zanzibar  pamoja na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.