Dkt. Kijaji : Zalisheni bidhaa za kuuza katika soko la AfCFTA

0
561

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amevitaka viwanda vyote nchini kutengeneza bidhaa zenye ubora na kwa gharama nafuu ili ziweze kuingia katika soko lililopo kwenye Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).

Waziri Kijaji ameyasema hayo alipotembea Kiwanda cha kuzalisha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga, kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji wa maziwa na kusikiliza na kutatua changamoto walizonazo.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali inafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha Wafanyabiashara na Wawekezaji wanakuwa na mazingira bora na wezeshi ili kufanya biashara kwa tija na kukuza uchumi wa Taifa