Wanawake watakiwa kujitokeza na kujenga uchumi

0
140

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Philip Mpango amewataka Wanawake nchini kuendelea kujituma na kuwa kichocheo cha kujenga Tanzania yenye maendeleo ya kiuchumi.

Dkt. Mpango.ambaye pia ni mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam ametoa wito huo wakati wa mkutano wake na Wanachama wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) wa mkoa huo.

Amesema mchango unaotolewa na Wanawake katika malezi, lishe bora na kulinda  maadili katika jamii ni mkubwa, hivyo pia wanaweza kuwa pamoja na ujenzi wa uchumi ni mkubwa, hivyo wanaweza
kuwa kichocheo cha kujenga Tanzania yenye maendeleo ya kiuchumi.

Dkt. Mpango pia amewasihi Wananchama wa UWT kutokana na ushawishi walionao kuwelimisha Wananchi ili washiriki katika sensa ya watu na makazi iliyopangwa kufanyika mwaka 2022.

Amesema ili kupata takwimu sahihi na kupanga mipango ya maendeleo, ni muhimu kwa Wananchi wote wakashiriki katika sensa hiyo.

Wakati wa mkutano huo, UWT mkoa wa Dar es salaam iliwasilisha ombi kwa mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango kuwa mlezi wake, ombi ambalo Mama Mbonimpaye ameliridhia.