Ofisi za vijiji, vitongoji, mitaa hazina hata maji ya kunywa

0
182

Mbunge wa jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara
ameitaka Serikali kuongeza posho kwa Wenyeviti wa vijiji, vitongoji, mtaa na Madiwani ili kuwawezesha viongozi hao kutekeleza majukumu yao.

Akichangia hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa Waitara amesema, katika mipango yote ya Serikali hakuna mahali bajeti inaonesha namna ambavyo viongozi wa ngazi ya vijiji, mitaa na vitongoji wanawezeshwa kufanya kazi zao.

Amedai kuwa posho za Madiwani mara ya mwisho kuongezwa ni mwezi Agosti mwaka 2012 miaka 12 iliyopita, japo ndio wanaobebeshwa majukumu katika meneo yao.