Hayati Karume afanyiwa Dua Kisiwandui

0
111

Raia wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi, leo Aprili 2024 amewaongoza wananchi na viongozi mbalimbali katika dua maalumu ya kumuombea Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Dua hiyo ambayo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, dini pamoja wananchi imefanyika katika ofisi kuu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui, Zanzibar, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Sheikh Karume aliyeuawa Aprili 7, 1972.

Miongoni mwa viongozi waliohudhuria dua hiyo ni Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Emmanuel Nchimbi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.