Watanzania kushiriki maonesho ya biashara China.

0
142

Baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania watashiriki maonesho ya biashara ya Kimataifa maarufu kama Canton Fair huko jijini Guangzhou nchini China. Wafanyabiashara hao wataongozwa na Mwandishi wa vitabu mkongwe nchini, Nyambari Nyangwine.

Maonesho hayo yanatarajiwa kuwa na manufaa mbalimbali kwa wafanyabiashara wa Tanzania ikiwamo kufungua fursa mbalimbali za kibiashara na ushirikiano wao baina ya Tanzania na China.