Vyuo vikuu visivyofuata vigezo kuwajibishwa

0
938

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema serikali itaendelea kuchukua hatua dhidi ya vyuo vikuu visivyofuata vigezo vilivyowekwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini –TCU.

Waziri Ndalichako amesema hayo alipozungumza na wakuu wa vyuo vikuu na vyuo vikuu vishiriki wanaokutana mjini Morogoro kujadili masuala mbalimbali ya uboreshaji elimu katika vyuo hivyo.