Simba yapigwa faini kisa ushirikina

0
445

Simba SC imetozwa faini ya shilingi Milioni moja kwa kosa la mashabiki na walinzi wake wa uwanjani kupanga njama na kufanikisha azma ya kuingia uwanjani na kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina katika mchezo.

Mashabiki hao wanadaiwa walionekana wakijadiliana na walinzi kabla ya kuingia uwanjani na kufanya kitendo hicho kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa FC katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam uliochezwa Machi 15 mwaka huu.

Walinzi waliofungiwa ni Kessy Mohamed, Mrisho Mindu na Mohamed Salmin pamoja na shabiki Mohamed Saleh ambao wamefungiwa kwa muda wa miezi 12.

Bodi ya Uendeshaji wa Ligi inaendelea na uchunguzi kubaini wahusika wengine ambao hawakutambulika ili nao wachukuliwe hatua.