Serikali kusambaza vifaa tiba vya zaidi bilioni14.9

0
223

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amezindua usambazaji wa vifaa tiba (nje ya vilivyopangwa kununuliwa kwenye Bajeti ya 2023/24) vitakavyosambazwa katika majimbo yote 214 nchini Tanzania.

Waziri Ummy amezindua usambazaji wa vifaa hivyo leo jijini Dares Salaam na kusema kuwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa fedha za nyongeza shilingi bilioni 14.9 Novemba 2023 za kununua vifaa hivvo ili kuendelea kuboresha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto.

Miongoni mwa vifaa ambavyo amepokea ni pamoja na vitanda vya wagonjwa 3,080, vitanda vya kujifungulia 1,000, magodoro 5,500, mashuka 36,808, pamoja na meza za vitanda 306.

“Tunategemea kupokea vifaa tiba vingine hivi karibuni ambavyo ni vitanda vya kujifungulia (4,280); vitanda vya kufanyia uchunguzi 4,280; mkoba wa vitu vya kujifungulia, 4,280; kabati za vitanda 6,420 na stendi ya dripu (6420),” amesema Waziri Ummy.

Amefafanua kuwa “vifo vya uzazi vimepungua kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2016 hadi vifo 104 kwa vizazi hai 100,000 ikiwa lengo la dunia ni Tanzania kupunguza vifo vva wajawazito kufikia vifo 70 kila vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2030.”