Serikali kufanya maboresho bwawa la Chamakweza

0
563

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema Wizara itafanya maboresho kwenye mradi wa ujenzi wa Bwawa la kunyweshea maji mifugo lililopo Chamakweza Mkoani Pwani ili liweze kutoa huduma iliyokusudiwa.

Waziri Ndaki ameyasema hayo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea Kijiji cha Chamakweza wilayani Chalinze mkoa Pwani kukagua ujenzi wa mradi huo ambapo kamati ilibaini kuwepo kwa mapungufu katika utekelezwaji wake.

Waziri Ndaki ameieleza kamati hiyo kuwa Wizara itajipanga upya katika utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja nakufanya mapitio ya mchoro na kuangalia namna ya utekelezaji wa ushauri na maelekezo yaliyotolewa na kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge.

Mradi huo wa ujenzi wa bwawa la Chamakweza ulianza 19 Julai, 2020 na kukamilika tarehe 15 Mei, 2021 kwa gharama ya shilingi milioni 671, bwawa hilo linauwezo wa ujazo wa lita milioni 108,169,400.