Sekta ya madini yakusanya maduhuli trilioni 1.9

0
236

Katiki kipindi cha Machi 2021 hadi Februari 2024, Wizara ya Madini imetekeleza jukumu la ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo ada za mwaka za leseni, ada za ukaguzi, ada za kijiolojia, mrabaha, faini, adhabu na malipo ya huduma za maabara.

Katika kipindi hicho cha miaka mitatu ya uongo za Rais Samia Suluhu jumla ya shilingi trilioni 1.9 zimekusanywa kutokana na vyanzo hivyo.

Ongezeko la maduhuli linaonesha kukua kwa sekta hiyo ambapo takwimu za wizara zinaonesha kuwa kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2022, sekta ilikua kwa kasi ya asilimia 7.3 hadi 10.9 na katika kipindi cha robo ya tatu (Julai – Septemba) ya mwaka 2023 sekta ilikua kwa asilimia 10.2 ikilinganishwa na kasi ya ukuaji wa asilimia 9.6 katika kipindi kama hicho mwaka 2022.

Ukuaji huo umeongeza mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa kutoka asilimia 6.7 mwaka 2020 hadi asilimia 9.1 mwaka 2022.

Ongezeko hilo la mchango wa madini kwenye Pato la Taifa unaakisi dhamira ya serikali kuhakikisha sekta hii inaimarika na kuweza kuchangia hadi asilimia 10 ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025