Rais Samia: Ajenda Rasilimali Watu ni Moyo wa Afrika

0
166

Rais Samia Suluhu Hassan amefungua mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Rasilimali Watu unaofanyika Dar es Salaam, na kusisitiza kuwa Rasilimali Watu ni kitovu cha mageuzi chanya barani Afrika.

Amesema kwa zaidi ya muongo mmoja sasa Afrika imepitia katika mchakato wa ukuaji wa sekta za uchumi, lengo likiwa ni kuondokana na uchumi tegemezi.

Rais Samia amewaambia washiriki wa mkutano huo kuwa Bara la Afrika bado lina changamoto nyingi zinazohitajika kushughulikiwa kwa haraka ikiwa ni pamoja na
uhaba wa chakula, umaskini uliokithiri na ukosefu wa usawa.

“Ajenda hii [Mtaji wa Rasilimali Watu] ndio moyo wa Bara la Afrika, mkutano utaamua ni wapi pakuwekeza zaidi. Hatuwezi kulikomboa bara letu kiuchumi kama hatutoendeleza rasilimali watu,” amesisitiza Rais Samia.

Mkutano huo umehudhuriwa na zaidi ya washiriki elfu mbili kutoka nchi takribani 44 za Afrika.