Maporomoko ya udongo Geita yafunika mashamba

0
280

Zaidi ya ekari sita za mashamba ya mazao mbalimbali katika Mtaa wa Nshinde, Kata ya Nyankumbu nje kidogo ya Mji wa Geita zimeharibiwa na maporomoko ya udogo ambayo yametokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Geita.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba amewaomba wananchi kuwa watulivu na kutofika katika maeneo hayo kutokana na kuwa na maji mengi ardhini.

Mkurugenzi wa Halmashauri wa Mji wa Geita, Yefred Myenzi amesema Kamati ya Maafa ya Halmashauri ya Mji itafika katika eneo hilo kufanya tathmini ya madhara yaliyojitokeza na hivyo akawaomba wananchi kuwa wakweli wakati wa kutoa taarifa zao.

Mtaalamu wa jiolojia kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML), Musa Kasano amewaondoa hofu wananchi kuwa kilichotokea siyo mlipuko wa volcano bali ni maji yaliyojaa ardhini kutafuta njia ya kutokea.