Makonda: Dhuluma kwenye ardhi inatisha

0
297

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amesema katika ziara yake, amebaini kuwepo kwa kiwango kikubwa cha watu kudhulumiwa ardhi nchini, hali inayosababisha migogoro ya ardhi isiyokwisha.

Makonda ameyasema hayo leo Machi 5, 2024 aalipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya ziara yake ya mikoa 20 ya Tanzania Bara.

Amesema kuna wananchi wengi wamelalamika kudhulumiwa ardhi kwa kupewa hati feki au kiwanja kimoja kuuzwa kwa watu zaidi ya mmoja.

“Wanaotapeli ardhi wana mitandao mikubwa inayowalinda. Naomba Waziri wa Ardhi afanye mapitio ya watendaji wa Sekta ya Ardhi kubaini wanaoshiriki kudhulumu wanyonge ili wachukuliwe hatua za kiutumishi,” ameongeza Makonda.