Lowassa arejea CCM

0
875

Mgombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ametangaza kurejea Chama Cha Mapinduzi -CCM.

Lowassa ametangaza uamuzi huo katika ofisi ya CCM Lumumba jijini Dar Es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Rais Dkt. John Magufuli ambaye alikuwepo katika tukio hilo ametoa wito kwa watanzania kudumisha amani, umoja, udugu na mshikamano na kujielekeza katika ajenda kuu ya ujenzi wa taifa, badala ya kupoteza muda kwa malumbano.

Katika hatua nyingine Rais Dkt. Magufuli amesema hatamvumilia kiongozi yeyote wa mkoa, wilaya au Halmashauri atakayebainika kuhusika kuwatoza ushuru ama tozo yoyote wajasiriamali wadogo waliopatiwa vitambulisho.

Rais Dkt. Magufuli amefafanua kuwa kiongozi atakayebainika kuwatoza wajasiriamali wadogo wenye vitambulisho atachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuvuliwa madaraka, na hivyo ametaka wajasiriamali hao wasibughudhiwe.