Korogwe wasubiri elimu ya uwekezaji wa bandari

0
182

Wakazi wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wamesema wapo tayari kupokea elimu itakayotolewa na Serikali kuhusu uwekezaji wa bandari, unaofanywa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Wananchi hao wametoa kauli hiyo mara baada ya mkuu wa wilaya ya Korogwe, Jokate Mwegelo kuwapa taarifa ya ujio wa Katibu Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo anayekwenda kwenye eneo lao maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya uwekezaji bandarini.

Mwegelo amesema jukumu kubwa la Serikali ni kuwahudumia Wananchi, kutengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji pamoja na kukuza uchumi wa mtu moja moja na Taifa kwa ujumla.