Kiwanda cha sukari cha Kilombero kilichopo mkoani Morogoro kinakusudia kujenga kiwanda kikubwa kitakacho gharamu kiasi cha shilingi bilioni 650 ili kuongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani milioni 1.2 zilizopo sasa hadi kufikia tani milioni 2.4 kwa mwaka.
Akizungumza katika mkutano wa wadau uliokuwa na lengo la kujadili upanuzi wa kiwanda hicho, Mkurugenzi wa mahusiano wa kiwanda hicho Joseph Rugaimkamu amesema ujenzi wa kiwanda hicho kipya utaenda sambamba na upanuzi wa mshamba ya miwa ya kiwanda pamoja na wakulima wan je ili kukidhi mahitaji ya sukari katika soko la ndani na nje ya nchi.
Amesema ujenzi wa kiwanda hicho utasaidia kuongeza upatikanaji wa sukari katika soko la ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dakta Stephen Kebwe amezitaka halmashauri za Kilosa na Kilombero kushiriki kikamilifu ili kufanikisha mchakato wa utekelezaji wa maagizo ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha sukari iliyopo nchini inajitosheleza .