Kigamboni wakabiliwa na wimbi kubwa la waraibu wa dawa za kulevya

0
183

Licha ya Mapambano yanayoendelea ya kudhibiti Dawa za Kulevya hapa nchini, wilaya ya Kigamboni bado inakabiliwa na wimbi la watu wanotumia dawa hizo na hivyo kupoteza nguvu kazi hasa vijana.

Takwimu za hivi sasa zinaonesha kuwa watu zaidi 600 hufika kliniki kwa ajili ya kupatiwa dawa za kukabiliana na uraibu wa dawa za kulevya wilayani humo kwa mwaka mzima.

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri amekagua ujenzi wa moja ya kituo kinachojengwa na serikali ya Tanzania na shirika la Global fund ambacho kitakuwa mahususi kwa ajili ya kuwahudumia watu wenye uraibu wa dawa za kulevya wilayani humo na kusema kuwa licha ya jitihada hizo lakini bado watu wanendelea kuathirika na dawa hizo.

Hata hivyo DC Msafiri akaelezea namna wanavyojipanga kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii ili iachane kabisa na matumizi ya Dawa za kulevya.

Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo cha kutolea matibabu kwa waraibu wa dawa za kulevya wilayani humo, Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hilo, Dkt. Charles Mkopachemba amesema kuwa, uwepo wa kituo hicho utapunguza adha kwa waathirika wa dawa za kulevya kufuata dawa za methadoni wilayani Temeke.