JK ashinda tuzo ya kiongozi bora

0
234

Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo ya kiongozi bora kwa mwaka 2023 katika Tuzo za Kiongozi Bora wa Afrika kwa Mwaka 2023 kama kiongozi bora wa mwaka katika amani na usalama Barani Afrika.

Alizungumza jijini Addis Ababa, Ethiopia wakati wa hafla ya kutolewa kwa tuzo hizo iliyoandaliwa na Jarida la Uongozi Afrika (ALM), Dkt. Kikwete ameshukuru kwa kutunukiwa tuzo hiyo na kuwasihi Waafrika wote kwenye nafasi za uongozi kutoa kipaumbele kwenye masuala ya kutatua changamoto zilizopo ikiwemo umasikini, chakula, mabadiliko ya tabianchi magonjwa, ujinga, migogoro ya kisiasa na vita.

“Ukweli ni kwamba, ni kwa heshima kubwa ninakubali kupokea tuzo hii. Naipokea, si tu kwa ajili yangu bali kwa niaba ya Waafrika wengine wengi wawe viongozi wa kisiasa, wenye ushawishi kiuchumi, viongozi wa dini, wanachama wa vikosi vya usalama, watumishi wa umma na wananchi wa kawaida ambao huamka kila siku na kufanya sehemu yao katika kulifanya Bara la Afrika kuwa sehemu nzuri zaidi ya kuishi,” Amesema Dkt. Kikwete.

Rais Mstaafu Kikwete ametunukiwa tuzo hiyo kufuatia mchakato uliojumuisha mapendekezo ya majina pamoja na kura zilizopigwa mtandaoni kwa wale waliopendekezwa, ambapo aiibuka na ushindi wa asilimia 60.

Pamoja naye, Mtanzania Jesca Nkwabi pia ametunukiwa tuzo ya uongozi bora.