HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII KUPATIKANA NJE YA NCHI

0
281

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Fatma Taufiki amesema kamati hiyo itaikumbusha Serikali kupeleka wataalamu wa Ustawi wa Jamii katika taasisi za umma ikiwemo kwenye ofisi za ubalozi ili kuhakikisha huduma za ustawi wa jamii zinapatikana hadi nje ya nchi.

Amesema huduma hiyo itawasaidia watoto wanaoasiliwa na hata baadhi ya Watanzania wanaofanya kazi ughaibuni ambao hufanyiwa vitendo vya unyanyasaji.

Akitoa salamu za kamati hiyo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii na kilele cha wiki ya Ustawi wa Jamii mkoani Dar es Salaam, Fatma amesema kamati hiyo pia inaendela kuikumbusha Serikali kuhusu suala la idara ya Ustawi wa Jamii kuwa huru.

Ameongeza kuwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii inaendela kuishauri Serikali kujenga ofisi za faragha ambazo zitakidhi mahitaji ya utoaji wa huduma za Ustawi wa Jamii pale zinapotolewa.