Finland yaipongeza Tanzania

0
838

Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland,- Timo Soini amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli za kupambana na rushwa na kusimamia uwajibikaji.

Waziri Soini ametoa pongezi hizo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga ambaye yupo nchini Finland kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Wakati mazungumzo yao, Mawaziri hao wamesisitiza umuhimu wa Tanzania na Finland kuboresha ushirikiano kwenye sekta mbalimbali zikiwemo za biashara, uwekezaji, mafunzo ya ufundi na  ajira kupitia sekta ya misitu.

Aidha, Waziri Soini ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuhifadhi wakimbizi na mchango mkubwa katika usuluhishi wa migogoro inayozikabili baadhi ya nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.

Katika kuhamasisha uwekezaji wa viwanda nchini, Balozi Mahiga amefanya mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara na Kampuni kubwa za biashara nchini humo.