Dkt. Mwinyi: Wazazi zingatieni Elimu

0
279

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Mwinyi,
amewataka wazazi na waumini wa dini ya kiislamu kuzingatia umuhimu wa suala la elimu kwao na watoto wao ili kujenga kizazi bora

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo baada ya sala ya Ijumaa iliyoswaliwa katika msikiti wa Abuu Ubadya uliopo Fuoni Meli Saba Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha Dkt. Mwinyi amewataka wazazi kuwahimiza watoto wao kusoma elimu zote mbili ikiwemo elimu ya dini na elimu ya dunia, kufanya hivyo itasaidia kuharakisha hatua za kimaendeleo.

Mbali na hilo Dkt.Mwinyi amesema moja ya sababu kuu za mmomonyoko wa maadili katika jamii ni kutokana na ukosefu wa elimu kwa jamii