Aaangukiwa na ukuta na kufariki dunia

0
248

Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine amejeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba waliyokuwa wakiishi katika kijiji cha Mboliboli
tarafa ya Pawaga, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Iringa.

Mvua hizo pia zimesababisha kaya 140 kukosa makazi huku miundombinu ya barabara na ile ya umwagiliaji kuharibiwa.

Kamati ya Usalama ya mkoa wa Iringa ikiongozwa na mkuu wa mkoa huo Halima Dendego imetembelea kata ya Pawaga kujionea uharibifu uliotokea na kutoa msaada kwa kaya zilizoathirika.

Dendego amewataka Wananchi wa Iringa kuendelea kuchukua tahadhari kutokana na mvua hizo zinazoendelea kunyesha.