Rais wa Namibia afariki dunia

0
640

Rais wa Namibia, Dkt. Hage Geingob (82) amefariki dunia leo Februari 04, 2024 katika Hospitali ya Lady Pohamba nchini humo alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimetolewa na Kaimu Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba, ambapo amesema familia ya kiongozi huyo ilikuwa pembeni yake wakati anafariki dunia.

Geingob ametumikia wadhifa huo kuanzia Machi 21, 2015.