Polisi mbaroni Kenya kwa biashara ya binadamu

0
266

Maofisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini Kenya wametiwa mbaroni baada ya maofisa wa upelelezi kuvamia nyumba ambayo Waethiopia 37 walikuwa wametunzwa, umbali wa kilomita 16 kutoka Jiji la Nairobi.

Askari waliokamatwa wanatuhumiwa kwa kushiriki biashara haramu ya kusafirisha binadamu.

Waethiopia hao wamewaambia maofisa upelelezi kwamba walikuwa njiani kuelekea Afrika Kusini kutafuta maisha bora, gazeti la The Star limeripoti.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, msako unaendelea kumtafuta mwenye nyumba hiyo pamoja na washirika wake wengine katika mtandao wa biashara ya binadamu.

Kenya inaelezwa kuwa njia maarufu wanakopitia wahamiaji haramu kutoka Ethiopia wanaojaribu kuingia Afrika Kusini kinyume cha sheria