NORDIC watakiwa kuwekeza kwa vijana Afrika

0
131

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba amezitaka nchi za NORDIC kutumia fursa za ushirikiano kati yao na Afrika kuwekeza kwenye nguvu-kazi ya bara hilo kwani ndilo lenye idadi kubwa ya vijana ikilinganishwa na Ulaya.

Makamba ameyasema hayo wakati akichangia hoja katika ufunguzi wa kikao cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NORDIC na Afrika, kilichofanyika jijini Copenhagen, Dernmark.

Amesena vijana wengi wa Afrika wamekuwa wakihama makazi yao na kwenda kutafuta kazi Ulaya mbali na vikwazo wanavyokutana navyo na kwamba suluhusho la kudumu la jambo hilo ni kuwekeza kwa vijana kule wanakotoka ili waweze kujiendeleza wakiwa nyumbani.

“Kutakuwa na shida ya wahamiaji hapo baadaye [Nchi za Nordic]. Ni vyema kuhakikisha kuwa vijana wanapata maarifa na ujuzi wa kuwasaidia huko walipo lakini pia hapo baadaye wanaweza kuja na kusaidia katika maendeleo ya nchi za Nordic kutokana na ujuzi mliowapatia,” amesema Waziri Makamba

Hoja hiyo imeungwa mkono na viongozi wengine wa Afrika wakizitaka nchi za NORDIC kuwekeza Afrika ili kupunguza usafirishwaji wa malighafi kwenda nje na kurudishwa kama bidhaa zinazoenda kuuzwa kwa bei kubwa yenye kukandamiza wazalishaji.

Nchi za NORDIC ni pamoja na Norway, Sweeden, Finland na Denmark.