Mabaki ya satelaiti kongwe kuanguka duniani

0
1146

Mabaki ya satelaiti ya kwanza ya Ulaya yanatarajiwa kuanguka duniani muda wowote kuanzia sasa, imefahamika.

Lengo la satelaiti hiyo ERS-2 iliyozinduliwa mwaka wa 1995 ilikuwa kuchunguza anga na kuunda teknolojia ambazo sasa zinatumika mara kwa mara katika kufuatilia sayari.

Imekuwa ikishuka hatua kwa hatua tangu kumalizika kwa shughuli yake mwaka 2011 na leo inachukua mkondo usio na udhibiti na hatari katika angahewa.

Shirika la Anga za Juu la Ulaya (Esa) linasema sehemu kubwa ya satelaiti hiyo ya tani mbili itaungua wakati ikishuka.

Baadhi ya sehemu zake zenye nguvu zaidi zinaweza kuhimili joto kali wakati inaposhuka kwa kasi ya juu, lakini uwezekano wa vipande hivi kuanguka maeneo yenye watu wengi na kusababisha uharibifu ni mdogo.

Vipande vyake vinaweza kutua popote duniani lakini kwa sababu sehemu kubwa ya dunia imefunikwa na bahari, matumaini ni kwamba mabaki yake yataanguka baharini.