Kichanga kilichookolewa Uturuki chaunganishwa na mama yake

0
219

Mtoto mchanga aliyeokolewa kwenye kifusi nchini Uturuki saa 128 baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi, ameunganishwa na mama yake mzazi Yasemin,
takribani miezi miwili baada ya tetemeko hilo.

Baada ya mtoto huyo mchanga aliyekuwa na wiki 14 kuokolewa, wauguzi walimpa jina la ‘Gizem’ yani ajabu.

Kabla ya mtoto huyo kuunganishwa na mama yake, vipimo vya vinasaba vilifanywa ili kuthibitisha kama kweli Yasemin ndiye mama halali wa Gizem, zikiwa zimepita siku 54 tangu wapotezane.

Baba mzazi wa Gizem pamoja na kaka zake wawili ni miongoni mwa watu waliofariki dunia kwenye tetemeko kubwa la ardhi lililotokea katika nchi za Uturuki na Syria ambapo zaidi ya watu elfu 50 walifariki dunia.