Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amefanya ziara nchini Ugiriki kuonyesha mshikamano na nchi hiyo baada ya kipindi kigumu cha kubana matumizi na kuipa msaada wa kidiplomsia kuhusu ubadilishaji wa jina wa taifa jirani la Macedonia.
Merkel pia amefanya mazungumzo na waziri Mkuu Alexis Tsipras kujadili hatua inayosubiriwa ya kubadili jina la taifa hilo la Macedonia iliyokuwa sehemu ya Jamhuri ya zamani ya Yugoslavia .
Merkel alizuru mji mkuu wa Macedonia, Skopje kabla ya kura ya maoni juu ya kubadili jina kuonyesha uungaji wake mkono ambapo bado suala hilo linasababisha mgawanyiko nchini Ugiriki ambako mojawapo ya vyama vinavyounda muungano wa Tsipras kinapinga na kutishia wingi wake wa bungeni.
Wakati huo huo polisi nchini Ugiriki imewatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi mamia ya waandamanaji waliokuwa wakipinga ziara hiyo ya Merkel