Facebook yapigwa stop

0
297

Serikali ya Eswatini imeiagiza kampuni kubwa ya mawasiliano nchini humo ya MTN kuufunga mtandao wa Facebook, ikiwa ni moja ya njia ya kukabiliana na maandamano ambayo yamedumu nchini humo kwa miezi kadhaa.

Habari kutoka nchini humo zinaeleza kuwa Serikali ya Eswatini imekuwa ikiwashutumu watumiaji wa mitandano mbalimbali ya kijamii nchini humo hasa Facebook kwa kueneza habari zisizo na uhakika, na hivyo kuchochea maandamano pamoja na ghasia nchini humo.
 
Katika barua yake aliyoiandikia kampuni hiyo ya MTN, Waziri wa Mawasiliano wa Eswatini, Princess Sikhanyiso amesema Serikali ina jukumu la kuhakikisha amani inakuwepo nchini humo, hivyo ni lazima mtandao huo wa Facebook ufungwe baada ya kudhihirika umekuwa ni sehemu ya kuchochea uvunjifu wa amani.
 
Tayari kampuni hiyo kubwa ya mawasiliano ya MTN imewajulisha watumiaji wake kuhusu agizo hilo la kufungwa kwa mtandao wa Facebook nchini Eswatini, hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
 
Tangu mwezi June mwaka huu, Eswatini imegubikwa na maandamano ambapo waandamanaji wanapinga utawala wa Kifalme