TCRA yaagizwa kushughukia malalamiko kuhusu bando na vifurushi

0
209

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndugulile ameipa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) muda wa miezi mitatu, kushughulikia malalamiko ya Wananchi kuhusu huduma za bando na vifurushi zinazotolewa na kampuni za simu za mkononi.

Dkt Ndugulile ameyasema hayo wakati wa ziara yake alipotembelea TCRA, ikiwa ni moja ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Ameitaka TCRA ishughulikie malalamiko ya Wananchi kwa kuwa kwa sasa hawana imani na bando na vifurushi na ameshauri kuwa na mfumo wa kuhakiki gharama halisi za mawasiliano kuendana na fedha aliyotoa Mwananchi na kuwe na namba ya bure ambayo Wananchi watapiga ili kuwasilisha malalamiko yao.

Dkt Ndugulile ameitaka TCRA kushirikiana a Baraza la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano ili kumaliza malalamiko hayo.

Pia ameiagiza TCRA kuhakikisha chaneli tano za bure za runinga zinaonekana hata baada ya muda wa kulipia kumalizika, kwa kuwa kwa sasa chaneli hizo hazionekani kwenye baadhi ya ving’amuzi.