MAMBO MATATU YALIYOCHANGIA KUONGEZEKA KWA MAPATO

0
6300

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha amefanya mahojiano maalum na Rais Samia Suluhu Hassan
Ikiwa ni mwaka mmoja tangu aingie madarakani, ambapo ametaja mambo kadhaa yanayochangia ongezeko la mapato.

TUMEONDOA HOFU KWENYE KUFANYA BIASHARA, TUMEWEKA MAZINGIRA MAZURI YA KUFANYA BIASHARA

“Kwanza tumeweka mazingira mazuri ya kufanya biashara, tumeondoa hofu ya kufanya biashara, nadhani wote ni mashahidi kwamba watu wengi wafanyabiashara kuna kipindi walifunga biashara zao, kwa hiyo kutokana na kuwahakikishia usalama wao katika biashara, biashara zimerudi.

Tumeweka mfumo mzuri TRA hakuna sasa ku harass mfanyabiashara, ame defolt mwite kaa naye kitako jua sababu zake kwa nini hakulipa kodi yake vizuri, mpe muda alipe kuliko kutishiana na mambo mengine kwa hiyo watu wanalipa”

UWEKEZAJI UNAONGEZEKA

“Watu wanakuja zaidi kuwekeza na wanapokuja zaidi tunatanua wigo wa kukusanya mapato”

MFUMO WA MAPATO

“Lingine ni kufanya mfumo wa mapato ueleweke usiwe wa kibabaishaji”