Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC) lateua mabalozi Tanzania

0
283

Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC) limewateua Watanzania watatu kuwa mabalozi wa baraza hilo nchini, ili kuhakikisha linatimiza wajibu wake ipasavyo na kufanya biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na nchi za Afrika Mashariki kushamiri bila vikwazo.

Walioteuliwa ni Raphael Maganga, Mtaalamu wa Diplomasia ya Uchumi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Mercy Sila, Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Wanawake Tanzania, na Dkt. Samuel Nyantahe, Mkurugenzi Mtendaji Daima Associates.

EABC iliundwa mwaka 1998 kama kiungo muhimu katika mkataba wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki (EAC Treaty) ambao ulilisisitiza ushiriki wa sekta binafsi ili kufikia maendeleo enedelevu ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Baraza hilo ndio mwamvuli wa vyama vyote vya biashara katika nchi zote saba za Jumuiya ya Afrika Mashariki.