Jux kukiwasha Kigoma

0
477

Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya katika miondoko ya RnB, Juma Musa almaarufu Jux anatarajia kufanya show ya muziki mkoani Kigoma.

Jux ambaye anatamba na nyimbo zake maarufu ukiwemo Uzuri Wako, Nitasubiri , Sisikii na Utaniua atawasili mkoani Kigoma Juni 26 mwaka huu ambapo kabla ya tamasha hilo atatembela chuo cha mafunzo Kigoma (KTC) kubadilishana mawazo na wanafunzi.

Wakizungumza na wanafunzi wa chuo hicho kamati ya uratibu ya tamasha hilo inayoongozwa na Grace Mbiro imesema Jux atatembelea chuo hicho ikiwa ni sehemu ya kutangaza muziki wake.