26 waokolewa ajali ya ndege Ziwa Victoria

0
773

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema kwamba ndege ya Precision Air iliyopata ajali katika Ziwa victoria ilikuwa na abiria 39 na wafanyakazi wa ndege 4, na hadi sasa watu 26 wameokolewa kutoka kwenye ajali hiyo iliyotokea mapema asubuhi ya leo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Chalamila amesema majeruhi hao wamefikishwa moja kwa moja katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kupatiwa huduma za afya

Chalamila amesema vikosi vya uokoaji vinaendelea na zoezi na kuokoa watu waliobaki katika ndege hiyo na kusema kuwa bado wana mawasiliano na rubani wa ndege hiyo ikiwa bado ipo ndani ya maji

Chalamila amesema vikosi vya uokoaji vinaendelea na zoezi hilo na wanaangalia kama ndege imegusa chini ili kupata utaalamu zaidi wa kuweza kuivuta na kuitoa nje ya maji

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwaombea ndugu na jamaa walioathirika na ajali hiyo huku wakiendelea kuwa watulivu na kusema kuwa ataendelea kutoa taarifa kuhusiana na ajali hiyo kila baada ya saa 2 kuona kama kuna jambo jipya limejitokeza