Home You and Your Family Mtama Cup yaanza kutimua vumbi

Mtama Cup yaanza kutimua vumbi

Mratibu wa mashindano ya Mtama, Seleman Mathew Timu 17 za mpira wa miguu na pete kutoka kata sita za  Tarafa ya Mtama, Halmashauri ya Lindi vijijini zimeanza kutimua vumbi  katika viwanja vya michezo vya Mtama kwa ajili ya kuwania kombe la Mtama Cup.

Mratibu wa mashindano hayo ambaye pia ni mdhamini Seleman Mathew amesema lengo la kuanzisha kombe hilo ni kukuza vipaji kwa vijana wenye uwezo wa  kusakata kabumbu.

Kwa upande wao vijana  wacheza soka wameomba wadau wa michezo kuangalia na mikoa ya kusini ambako kuna vijana wenye vipaji.

Mashindano hayo yanatarajiwa kufungwa na  waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mtama Bernad Membe na washindi watakabidhiwa vikombe na zawadi mbalimbali.

Martina Ngulumbi, TBC Lindi.

Last Updated ( Thursday, 30 August 2012 12:16 )  
Banner