Mabondia Francis Cheka na Japhet Kaseba wamekubaliana kupigana katika pambano lisilo la ubingwa la tamasha la matumaini lililopangwa kufanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam jumamosi wiki hii.

Mabondia hao walikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia pambano hilo na kusema kuwa tamasha hilo ni la kuchangisha fedha za ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike katika mikoa 8 ya Tanzania.
Upande wa wanawake wasanii wa filamu Jackline Wolper atapanda jukwaani kuzichapa na Wema Sepetu.
Mbali na ngumi hizo kutakuwa na pambano la wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa soka ambapo wabunge wanaoshabikia Simba na Yanga watacheza katika mchezo huo na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali zitakuwepo.

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)