Home You and Your Family Simba yakanusha okwi kusajiliwa Yanga

Simba yakanusha okwi kusajiliwa Yanga

Mchezaji wa Simba, Mganda Emmanuel OkwiKlabu ya Simba imekanusha juu ya mchezaji wao Mganda Emmanuel Okwi kwamba amesajiliwa na klabu ya Yanga msimu wa ligi kuu 2012/2013  na kudai kuwa bado ni mchezaji wao halali.

Akizungumza na waandishi wa habari makamu mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange ameeleza kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya vyombo vya habari kuandika mambo ya uongo na kwamba mchezaji huyo kwa sasa yuko Uganda akijiandaa kwenda nchini Italia kwa majaribio.

Nyange ameonyesha mkataba wa mchezaji huyo ambao ulisainiwa mwaka jana na kuwa utaisha mwaka 2013.

Last Updated ( Friday, 06 July 2012 11:33 )  
Banner