Home You and Your Family Mahiza afungua kambi ya UMISETA Pwani

Mahiza afungua kambi ya UMISETA Pwani

Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mwantum  Mahiza Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantum  Mahiza amefungua kambi ya michezo kwa wanafunzi wa shule za sekondari mkoa wa Pwani wanaojiandaa kushiriki katika mashindano ya umoja wa michezo ya shule za sekondari UMISETA kanda ya Mashariki na kuwataka wanafunzi watakaoshiriki mashindano hayo kuzingatia suala la nidhamu wakati wote.

Akizungumza na wanafunzi hao katika viwanja vya shule ya sekondari Filbart Bay iliyopo katika halmashauri ya mji wa Kibaha Mahiza  amesema katika kipindi cha siku tatu  ambacho wanafunzi hao watakaa kuandaa timu ya mkoa itakayoshiriki michuano ya kanda kigezo kikubwa kitakachoangaliwa kuchukua wachezaji ni pamoja na nidhamu kwa washiriki na ukakamavu.

Hali kadhalika, Mkuu huyo wa mkoa amewataka maafisa elimu wanaosimamia kambi hiyo kuhakikisha kuwa wanamichezo wanapatiwa chakula kinachojenga mwili ili kuweka miili yao katika stamina nzuri ya kuweza kuhimili michuanao.

 Joseph Chewale, TBC Pwani.

Last Updated ( Thursday, 07 June 2012 12:12 )  
Banner