Home You and Your Family Makocha na waamuzi 57 wa kuogelea kunolewa Na FINA

Makocha na waamuzi 57 wa kuogelea kunolewa Na FINA

Mkufunzi kutoka shirikisho la dunia la mchezo wa kuongelea FINA, Gerd Nottelmann Makocha na waamuzi 57 wa mchezo wa kuogelea wanatarajiwa kuhudhuria mafunzo ya siku kumi ya mchezo huo ambayo yataendeshwa na mkufunzi kutoka shirikisho la dunia la mchezo wa kuongelea FINA, Gerd Nottelmann kutoka Ujerumani.

Kozi hiyo inatarajiwa kuanza leo jumatatu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalim Julius Nyerere, mkufunzi Nottelman na Katibu Mkuu wa shirikisho la mchezo wa kuogelea nchini Nicolous Kihunsi wamewataka makocha hao kutumia mafunzo hayo kuibua vipaji na kuviendeleza kwa wachezaji chipukizi.

Makocha hao 57 wanatoka katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam.

Last Updated ( Monday, 04 June 2012 10:45 )  
Banner