Home Technology DRC yatoa angalizo waasi kuingia karibu na Goma

DRC yatoa angalizo waasi kuingia karibu na Goma

Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo imetoa angalizo kuwa kundi la waasi limefanikiwa kuingia katika  eneo la karibu na mji wa Goma nchini humo karibu kabisa na mpakani mwa nchi hiyo na Rwanda.

Hali hiyo inawafanya ya wananchi waishio katika mji huo wa Goma kuyakimbia makazi yao ili kuokoa maisha na baadhi ya mali zao.

Serikali ya DRC pamoja na umoja wa mataifa unailaumu Rwanda kuwa inawasaidia waasi hao, madai ambayo serikali ya Rwanda imeyakanusha.

Wakati huo huo, mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai The Heague imemhukumu kifungo cha maisha kiongozi wa kundi la waasi la Congo, Toma Lubanga.

Adhabu hiyo ya kifungo cha miaka kumi na minne inatokana na Lubanga kupatikana na hatia ya kuwatumia watoto chini ya umri wa miaka kumi na mitano katika vita katika kundi hilo la waasi.

Last Updated ( Wednesday, 11 July 2012 10:49 )  
Banner