Home Technology Makao makuu ya kampeni ya mgombea urais yashambuliwa Misri

Makao makuu ya kampeni ya mgombea urais yashambuliwa Misri

Mgombea Urais wa Misri, Ahmed Sharif Makao makuu ya kampeni za mgombea Urais wa Misri Ahmed Sharif yameshambuliwa muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yaliyoonesha kuwepo kwa duru ya pili ya uchaguzi nchini humo.

Televisheni ya Taifa nchini humo imeonesha picha za jengo hilo lililopo katika wilaya ya Dokki katika mji mkuu wa Cairo likiwa linawaka moto.

Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za watu waliojeruhiwa wala kupoteza maisha kutokana na shambulio hilo.

Shambulio hilo limetokea saa chache baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi ambapo mgombea huyo Sharif ametangazwa kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi itakayofanyika mwezi ujao.

Ingawa mpaka sasa hakuna taarifa za nani aliyeendesha shambulio hilo lakini inaelezwa kuwa washambuliaji hao waling’oa mabango ya kampeni ya Sharif na kuingia ndani ya jengo hilo na kuchukua baadhi ya kompyuta.

Last Updated ( Tuesday, 29 May 2012 12:13 )  
Banner