Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Listen TBC Live
      TBC Taifa
      TBC FM
Home Technology Jeshi la Marekani laokoa mateka wa kigeni Somalia

Jeshi la Marekani laokoa mateka wa kigeni Somalia

Jessica Buchanan toka Marekani na Poul Thisted toka CanadaJeshi la Marekani limefanikiwa kuwaokoa raia wawili wa kigeni ambao ni wafanyakazi wa mashirika ya misaada wanaofanya kazi katika eneo la Galkayo nchini Somalia waliokuwa wametekwa na maharamia wa Kisomali.

Maharamia hao wa kisomali waliwateka raia hao wa kigeni na kuendelea kuwashikilia kwa kipindi cha miezi mitatu. Raia hao wa kigeni ambao ni Jessica Buchanan kutoka nchini Marekani na Poul Thisted raia wa Canada wameokolewa na helikopta ya jeshi la Marekani.

Helikopta hiyo ililazimika kuwashambulia marahamia hao wa kisomali na jeshi la Marekani inasemekana limefanikiwa kuwaua maharamia wanane na kuwakamata maharamia wengine watano.

Last Updated ( Wednesday, 25 January 2012 16:12 )  
Banner