Home Local General Pinda akemea mauaji ya vikongwe, Albino Geita

Pinda akemea mauaji ya vikongwe, Albino Geita

Waziri mkuu Mizengo PindaWaziri mkuu Mizengo Pinda amekemea mauaji ya wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) ambayo  yamekuwa  yakijitokeza kwenye mikoa ya kanda ya ziwa licha ya jitihada za serikali za kuzitokomeza.

Akiwahutubia wananchi katika wilaya ya nyang’hwale mwanzoni mwa ziara yake ya siku tatu mkoani Geita, Pinda amesema vitendo hivyo  havikubaliki na kuwataka wananchi kuwafichua watu wanaoviendeleza.

Pinda amefanya mkutano wake mkubwa wilayani Nyang’hwale kuhamasisha wananchi kuitumia fursa ya eneo hilo kuwa katika mkoa mpya na wilaya mpya kujiletea maendeleo kwa kasi zaidi.

Waziri mkuu Pinda amesisitiza juu ya umuhimu wa kukuza uchumi wa wananchi  hao kwa kutumia rasilimali walizonazo ikiwemo aridhi.

Mapema  akitoa taarifa mkuu wa mkoa wa Geita  magalula Saidi Magalula ametaja baadhi ya changamoto zinazoukabili mkoa huo kuwa ni uhaba wa watumishi, majengo wataalamu wa afya  na huduma nyinginezo zikiwemo za kifedha.

Waziri mkuu Mizengo Pinda leo anaendelea na ziara yake  katika wilaya ya Geita kabla ya hapo kesho atakapoendelea na ziara katika mkoa wa mwanza ambako atafungua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

Estom Sanga, TBC Geita.

Last Updated ( Monday, 10 September 2012 10:49 )  
Banner