Home Local General Simbachawene aitaka TPDC kuondoa sumu shimoni Kilwa

Simbachawene aitaka TPDC kuondoa sumu shimoni Kilwa

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene Naibu Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene ametembelea visima vya gesi asili na mtambo wa kusafishia gesi ya Songosongo katika wilaya ya Kilwa na kulitaka shirika la mafuta la maendeleo nchini- TPDC- kuondoa sumu iliyohifadhiwa ndani ya shimo.

Simbachawene amesema hayo baada ya kupata kilio kutoka kwa wakazi wa Songosongo kufuatia kuwepo kwa shimo lililohifadhi kemikali  na kampuni ya Ndovu wakati wa uchimbaji wa gesi  na kusababisha mifugo ya wakazi hao  kufa baada ya kunywa maji yanayotoka katika shimo hilo wakati wa mvua na kuingia katika vyanzo vya maji.

Visima vya gesi vya Songosongo vilianza kufanyiwa utafiti miaka 54 iliyopita na kuanza kuchimba gesi mwaka 1974 kwa kupata kisima kimoja lakini hivi sasa kuna jumla ya visima 11 na saba kati yao ndiyo vinafanya kazi ya utoaji wa gesi vitatu vikiwa baharini na vinne vikiwa nchi kavu.

Martina Ngulumbi, TBC Lindi.

 

Last Updated ( Monday, 10 September 2012 10:14 )  
Banner