Home Local General Wafanyabiashara manispaa ya Morogoro waomba kuendesha Masoko

Wafanyabiashara manispaa ya Morogoro waomba kuendesha Masoko

Mkurugenzi wa manispaa ya morogoro, Jarvis Sembeye Wafanyabiashara katika masoko ya manispaa ya Morogoro wameiomba manispaa hiyo kuwapatia fursa ya kusimamia masuala ya uendeshaji wa masoko hayo ili kuboresha hali ya usafi.
 
Wakizungumza katika mkutano uliwakutanisha wafanyabiashara pamoja na viongozi wa manispaa ulioandaliwa na chama cha wafanyabiashara na viwanda TCCIA  ili kujadili matatizo yaliyopo kati yao na manispaa, wamesema majukumu wanayotaka wapewe ni pamoja na ukusanyaji wa mapato na kusimamia huduma mbalimbali za kijamii zilizopo katika masoko hayo.

Wafanyabiashara hao wamesema iwapo uongozi wa manispaa ya morogoro utakuwa tayari kuwapatia fursa hizo , watazitumia kujenga vyoo na kusimamia usafi wake, kuhakikisha huduma ya maji inapatikana muda wote na kuhakikisha usafi wa soko unazingatiwa wakati wote tofauti na sasa.

Mkurugenzi wa manispaa ya morogoro Jarvis Sembeye pamoja na mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Morogoro Batchou Batchou wameelezea umuhimu wa kuendesha biashara bila ya kuwa na migongano na serikali.

Praxeda Mtani, TBC Morogoro.

Last Updated ( Friday, 31 August 2012 10:14 )  
Banner