Home Local General Polisi yaua mtuhumiwa wa ujambazi Arusha katika pambano la kurushiana risasi

Polisi yaua mtuhumiwa wa ujambazi Arusha katika pambano la kurushiana risasi

Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabasi Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limemuua mtu momja anayesadikiwa kuwa ni jambazi katika majibizano ya kurushiana risasi katika eneo la Daraja mbili majira ya saa tano usiku ambapo mwenzake alifanikiwa kukimbia.

Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Arusha Lebaratus Sabasi amewaambia waandishi wa habari kuwa walipata taarifa za kuwepo watu wanaoshukiwa kuwa majambazi na raia wema na Polisi walipo fika eneo la tukio wakaanza kushambuliwa na watu hao.

Kamanda Sabasi amesema kuwa mara vijana wake walipofika na kuanza kuwafuatilia watuhumiwa hao walianza kushambuliwa kwa risasai  na wao wakajibu ndipo mtuhumiwa mmoja alipopigwa risasi iliyosababisha kifo chake.

Wakati huohuo Jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja, ambaye anadaiwa kuwa ni katibu wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Endulen wilayani Ngorongoro, Denis Paulo kwa kujaribu kuwatapeli wafanyakazi wawili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kiasi cha Sh milioni 16.

 Kwamujibu wa kamanda Sabasi Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani  mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Khalifa Mshana, TBC Arusha.

Last Updated ( Friday, 31 August 2012 10:07 )  
Banner